Albert Schweitzer
Mandhari
Albert Schweitzer (14 Januari 1875 – 4 Septemba 1965) alikuwa mwanateolojia, mwanafalsafa, mwanamuziki na daktari kutoka eneo la Alsatia, ambalo lilikuwa sehemu ya Ujerumani kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, lakini la Ufaransa baadaye. Mwaka wa 1952 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobeli ya Amani kwa ajili ya falsafa yake. Hasa anajulikana kwa kuanzisha na kuongoza kituo cha kimisionari na hospitali eneo la Lambarene nchini Gabon.