Frank Zappa
Frank Vincent Zappa (21 Desemba 1940 - 4 Desemba 1993) alikuwa mwanamuziki na mtunzi kutoka nchini Marekani. Alijulikana kwa mtindo wake wa muziki, ambao mara nyingi ulikuwa wa ajabu na wa kuchekesha. Alitunga aina mbalimbali za muziki na albamu nyingi. Zappa alishirikiana na wanamuziki wengine wengi, haswa kundi lake la miaka ya mwongo wa 1960 The Mothers of Invention[1] na rafiki yake mwimbaji wa blues Captain Beefheart[2]. Watu wengine walimtaja kati ya watunzi bora katika muziki wa pop au hata muziki wowote usio wa classical[3][4].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Zappa alizaliwa mjini Baltimore, Maryland na wazazi wahamiaji kutoka Italia, lakini alitumia muda mwingi wa maisha yake kusini mwa Kalifornia[5]. Alikulia Baltimore, Florida, na Monterey, Claremont na El Cajon, Kalifornia.
Zappa alizaa watoto wanne na mkewe Gail. Waliwapa wote majina yasiyo ya kawaida sana: Moon Unit, Dweezil, Ahmet, na Diva.
Zappa alipinga waziwazi madawa ya kulevya[6], mahubiri ya runinga, na namna zote za kudhibiti muziki.
Zappa alifariki dunia kutokana na saratani ya kibofu huko Los Angeles, Kalifornia.
Tovuti za nje
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Interview with Frank Zappa", UMRK, Los Angeles, California: BBC [TV Show], March 1993.
- ↑ Miles, Barry (2004). Frank Zappa. London: Atlantic Books. ISBN 978-1-84354-092-2.
- ↑ Menn, Don (1992). "From the Editor". Katika Menn, Don (mhr.). Zappa! Guitar Player Presents. San Francisco, CA: Miller Freeman. uk. 3. ISSN 1063-4533.
- ↑ Isler, Scott (Februari 1994). Frank Zappa.
{{cite book}}
:|work=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mendoza, Bart (Novemba 11, 2005). "Counter Culture Coincidence" (PDF). San Diego Troubadour. uk. 4. Iliwekwa mnamo Septemba 11, 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Interview by Bob Marshall, October 22, 1988 – Part 03". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Februari 23, 2013. Iliwekwa mnamo Oktoba 3, 2016.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)