Miereka
Mandhari
Miereka ni michezo ya kupambana unaohusisha mbinu mbalimbali. Ili ushinde mapambano hayo ni lazima umwanɡushe au umdondoshe mwenzako unayepambana naye chini. Mchezo huu pia unaweza kuleta furaha kubwa kwa watazamaji wanaoupenda.
Mara nyinɡi mapambano hayo huhushisha watu wawili.
Kuna aina mbili za mchezo huu ambayo ni miereka ya kijadi na miereka ya kisasa. Sheria za kijadi katika mchezo huu hutofautiana na za kisasa na hiyo ndiyo sababu mojawapo iliyofanya mchezo kuwekwa katika sehemu mbili ambazo ni ya kijadi na kisasa.
Baadhi ya mbinu za kupigana katika mchezo huu zinatumika katika vikosi vya kijeshi mbalimbali hapa duniani, lakini katika mchezo huo hatutumii silaha za moto.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Miereka kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |