Nenda kwa yaliyomo

Milano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Milan)
Sehemu ya mji wa Milano


Milano
Milano is located in Italia
Milano
Milano

Mahali pa Milano katika Italia

Majiranukta: 45°27′00″N 09°11′00″E / 45.45000°N 9.18333°E / 45.45000; 9.18333
Nchi Italia
Mkoa Lombardia
Wilaya Milano
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 1,308,975
Tovuti:  http://www.comune.milano.it/
Uwanja wa duomo

Milano (pia Milan) ni mji mkubwa wa Italia ya kaskazini mwenye wakazi milioni 1.3. Rundiko la mji lina wakazi milioni 7.5. Ni mji mkuu wa eneo la Lombardia na kitovu cha uchumi na utamaduni.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa mnamo 400 KK na Wakelti ukawa mji wa Kiroma mnamo 222 KK ukajulikana kama Mediolanum. Mji ulikua katika Dola la Roma. Mwaka 293 Kaisari Diokletiano alichagua Milano kama mji mkuu wa nusu ya magharibi ya Dola la Roma. Tamko la MIlano lilitolewa 313 na makaisari Licinius na Konstantino Mkuu likatangaza mwisho wa mateso dhidi ya Wakristo.

Baada ya mwisho wa Dola la Roma katika magharibi mji uliharibiwa mara mbili na Wahunni na Waostrogothi wakati wa uhamisho wa Wagermanik. Ukatekwa tena na Walongobardi wahamiaji na kuwa mji mkuu wao. 774 uliingizwa katika himaya ya Karolo Mkuu ukaendelea kama sehemu ya falme za Wafranki, Wajerumani na Habsburg kwa karne nyingi.

Katika karne ya 19 wenyeji walidai kijitawala kama Waitalia na baada ya vita ya Sardinia na Ufaransa dhidi ya Austria Lombardia yote ikawa sehemu ya ufalme wa Sardinia-Piemonte ulioendelea kuwa Ufalme wa Italia.

Katika Italia mpya Milano ulikuwa kitovu cha uchumi. Ujenzi wa reli ulianzisha upanuzi wa viwanda. Milano ikawa mji wa viwanda na kukua haraka. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Benito Mussolini alianzisha harakati ya kifashisti mjini Milano.

Umuhimu wa Milano katika Italia

[hariri | hariri chanzo]

Leo hii Milano ni mji wa pili katika Italia. Benki kubwa za nchi zina makao makuu hapa pia soko la hisa la Italia. Kuna viwanda vingi pamoja na kampuni ya magari ya Alfa Romeo na kampuni ya matairi Pirelli. Pia mji huu ni makao makuu ya vyombo vya habari mbalimbali kama Mediaset na magazeti kama Il corriere della sera. Mji huu pia ni kitovu cha michezo mbalimbali. Una uwanja wa Giuseppe Meazza (San Siro) wenye uwezo wa kubebe watazamaji zaidi ya 80,000 ambao ndio mkubwa kuliko vyote nchini Italia. Pia kuna timu mbili za mpira wa miguu, Internazionale na AC Milan ambazo ni moja ya vilabu vinavyoheshimika duniani. Milano huitwa mji mkuu wa mitindo ya mavazi ya Italia.

Mji unajulikana sana kwa opera yake inayoitwa "Scala". Jengo mashuhuri ni kanisa kuu au "duomo".

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milano kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.