Mji Mkongwe
Mji Mkongwe (kwa Kiingereza: Stone Town) ndio sehemu ya kale ya Jiji la Zanzibar, mji mkubwa wa kisiwa cha Unguja na mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Kama kitovu cha historia yake kilichoathiriwa na utamaduni wa Waarabu, wa Waajemi, wa Wahindi na wa Wazungu, Mji Mkongwe umeandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).
Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu mwaka 1830, wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja.
Kati ya majengo maarufu ni Beit al Ajaib (Jumba la Maajabu lililobomoka tarehe 24 Desemba 2020[1]), Jumba la Sultani, Ngome Kongwe, Kanisa Kuu la Anglikana lililojengwa mahali pa soko la watumwa na hasa nyumba nyingi za kihistoria za ghorofa zilizojengwa na familia za tabaka la matajiri Waarabu zenye milango yenye mapambo mazuri.
Mji Mkongwe unapokea watalii wengi kila mwaka.
Mji wa kisasa umekua sana ng'ambo ya Mji Mkongwe.
Picha
[hariri | hariri chanzo]
-
Nyumba ya Maajabu (Beit-al-Ajaib)
-
Boma la Kale katika Mji Mkongwe
-
Mahali pa kuogelea ufukoni karibu na Mji Mkongwe
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya miji ya kale ya Waswahili
- Maeneo ya Kihistoria ya Kitaifa ya Tanzania
- Orodha ya Urithi wa Dunia katika Afrika
- Aga Khan Jamaat Khana, Zanzibar
- Bafu za Hamamni, Zanzibar
- Bustani za Forodhani, Zanzibar
- Jengo la Bharmal, Zanzibar
- Msikiti wa Malindi, Zanzibar
- Nyumba ya Tippu Tip, Zanzibar
- Soko la Darajani, Zanzibar
- Ubalozi Mdogo wa Uingereza, Zanzibar
- Zahanati ya Ithnashiri
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Stone Town travel guide kutoka Wikisafiri
- Historia na utamaduni wa Zanzibar Archived 7 Februari 2006 at the Wayback Machine.
- UNESCO Stone Town Site
- Stone Town Conservation and Development Authority Archived 22 Oktoba 2016 at the Wayback Machine.
- Zanzibar Urban District Homepage for the 2002 Tanzania National Census Archived 18 Machi 2004 at the Wayback Machine.
- Stranger in Paradise: Searching for a Place to Call Home in Stone Town Archived 18 Julai 2011 at the Wayback Machine. by Christopher Vourlias, World Hum, June 15, 2009
- Zanzibar Stone Town & Hotels Archived 11 Juni 2011 at the Wayback Machine. A travel guide website containing pictures and information about Stone Town as well as a selection of Stone Town Hotels.
- Stone Town sites and attractions Archived 16 Machi 2012 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mji Mkongwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |