Historia
Historia (kutoka Kigiriki ιστορια, historia; pia "tarehe" kutoka Kiarabu تاریخ tarih kwa maana ya "historia": pia tena "mapisi") ni somo kuhusu maisha ya binadamu na utamaduni wao wakati uliopita.
Mara nyingi neno hilo lina pia maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu (kwa mfano "historia ya ulimwengu").
Historia ni hasa mfululizo wa habari za mambo yaliyotokea pamoja na sababu zake.
Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani.
Historia inatufundisha kuishi: kumbukumbu za mambo ya zamani (vita, uhuru, viongozi na mengineyo) zinatuwezesha kuendelea vizuri zaidi.
Wanahistoria wanapata maarifa yao kutoka maandishi ya zamani (hasa kwa historia andishi), kutoka fasihi simulizi na kutoka akiolojia (hasa kwa historia ya awali).
Kurasa zinazohusiana
[hariri | hariri chanzo]- Historia ya Afrika[1]
- Historia ya Amerika
- Historia ya Asia
- Historia ya Australia
- Historia ya Ulaya
- Historia ya Wokovu
- Historia ya Kanisa
- Historia ya teolojia
- Historia ya utawa
- Historia ya Kanisa Katoliki
- Historia ya Uislamu
- Miaka
- Vita
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |