Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Tabianchi na mazingira

Familia wakipitia maji ya mafuriko ili kufikia kituo cha maji kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani huko Dikwa katika Jimbo la Borno kaskazini-mashariki mwa Nigeria.
© UNHCR

Chukua hatua sasa kwa ajili ya Afrika yenye mnepo tunayoitaka: UNDRR

Jukwaa la tisa la Kikanda la Afrika kwa ajili ya Kupunguza hatari za majanga linaendelea mjini Windhoek, Namibia, likiwa na kaulimbiu ya "Chukua Hatua Sasa kwa Ajili ya Afrika Yenye Mnepo Tunayoitaka." Mkutano huu wa siku nne umeandaliwa na serikali ya Namibia kwa kushirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza hatari za majanga (UNDRR) na Kamisheni ya Umoja wa Afrika, kwa ushirikiano na Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC).

Kipepeo aina ya monarch hukusanya nekta kutoka kwenye mmea wa mbigili (thistle plant).
Unsplash/Sean Stratton

Bioanuwai: Ni nini, na tunawezaje kuilinda?

Umoja wa Mataifa na wadau wake ulimwenguni wanakabiliana na upotevu mkubwa wa wanyama na mimea, tarehe 23 Januari wanakutana jijini Nairobi, kenya kujadili jinsi ya kuepuka upotevu huo, katika mkutano mkuu ambao utaangazia bioanuwai ni nini, na jinsi gani Umoja wa Mataifa, unaweza kusaidia juhudi za kuwezesha asili kuishi na kustawi.

Shamba la mahindi lililoharibiwa na ukame nchini Zambia, mojawapo ya nchi ambazo zimetangaza hali ya dharura huku likikabiliana na athari za El Niño.
© WFP/Nkole Mwape

Mamilioni ya watu wako hatarini kukosa chakula Kusini mwa Afrika: WFP

Eneo la Kusini mwa Afrika linakabiliwa na ukame wa kihistoria na janga kubwa zaidi la chakula ambalo limeathiri zaidi ya watu milioni 27 katika eneo hilo, ameeleza Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP, Tomson Phiri na akizungumza leo Oktoba 15 kwenye mkutano wa waandishi wa habari  katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi.

Athari zilizoachwa na tsunami nchini Indonesia
© UNICEF/Arimacs Wilander

Elimu ndio muhimili katika kupunguza hatari za majanga: UN

Leo katika Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Hatari za Maafa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuhakikishia kwamba vijana wana ujuzi na maarifa ili kutengeneza mustakabali unaojali mazingira  na wenye mnepo dhiidi ya mabadiliko ya tabianchi, wakatiiikielezwa kuwa hasara ya kila mwaka iliyosababishwa na majanga ya asili ilifikia dola bilioni 131 katika kipindi  cha miaka saba.