Terakota
Terakota ni sanaa na vifaa vya ufinyanzi vinavyotengenezwa kwa kutumia udongo mwekundu unaochomwa, mara nyingi bila ganda la kioo usoni mwake. [1] [2] [3] [4] [5]
Jina limetokana na neno la Kiitalia terracotta ("udongo uliochomwa"). Kimsingi hakuna tofauti kubwa kati ya matofali ya kuchomwa na terakota, ila kazi za terakota ni lazima kutekelezwa kwa umakini zaidi na kuchagua vema udongo unaofaa.
Mifano ya kazi za terakota ni pamoja na sanamu, vyombo vya mapambo, picha kwenye uso wa vyombo, pia sura ya mapambo ya nyumba, lakini pia vifaa sahili kama mabomba ya ufinyanzi kwa ajili ya maji.
Mifano mashuhuri sana ni sanamu za tamaduni za kale zilizodumu miaka elfu kadhaa kwa sababu udongo wa ufinyanzi, kama uliteuliwa vema na kuchomwa vema, utadumu karne nyingi. Kati ya mifano mashuhuri ni sanamu za "Jeshi la Terakota" pale China, sanamu za Nok na terakota za Ugiriki ya kale.
Rangi ya vifaa visivyotiwa ganda la kioo mara nyingi ni nyekundu-kahawia; kuna pia mifano ya njano inayotumia udongo tofauti.
Terakota inapokea rangi lakini haiwezi kung'aa hadi kuchomwa mara ya pili ambako uso wa nje hufunikwa na tabaka la kioo.
Picha za kazi za terakota
[hariri | hariri chanzo]-
Sehemu ya sanamu kutoka Misri ya Kale, inayoonyesha huzuni ya mungu Isis akiomboleza kumpoteza Osiris (Nasaba ya Kumi na Nane, Misri ya Kale ) Musée du Louvre, Paris
-
Jeneza la Kietruski kwenye makumbusho, ya Waetruski, mjini Roma, Italia
-
Sanamu ya mwanamkwe, kutoka Ugiriki ya Kale, mnamo 325–150 KK
-
Indian terracotta figures, Gupta dynasty
-
Kaburi la kifalme, Nasaba ya Han, China
-
British Museum, Seated Luohan from Yixian, from the Yixian glazed pottery luohans, probably of 1150–1250
-
Maximilien Robespierre, unglazed bust by Claude-André Deseine, 1791
-
Mapambo ya terakota iliyotiwa rangi na tabaka la kioo, katika nyumba ya Mji Haramu, Beijing.
-
Hekalu ya terakota Bishnupur, Uhindi
-
Hekalu ya Kihindu, 1739, Kalna, India
-
Sura ya Jengo la Simu la Bell Edison, Birmingham, England linaonyesha uzuri wa terakota.
-
Natural History Museum inaonyesha uso wake wa terakota unaopendeza
-
Modern painted horses beside a sacred tree, Tamil Nadu, India
-
Sanaa ya terakota ya kisasa, Bankura, West Bengal, India
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Merriam-Webster.com
- ↑ ‘Diagnosis Of Terra-Cotta Glaze Spalling.’ S.E. Thomasen, C.L. Searls. Masonry: Materials, Design, Construction and Maintenance. ASTM STP 992 Philadelphia, USA, 1988. American Society for Testing & Materials.
- ↑ ‘Colour Degradation In A Terra Cotta Glaze’ H.J. Lee, W.M. Carty, J.Gill. Ceram.Eng.Sci.Proc. 21, No.2, 2000, p.45-58.
- ↑ ‘High-lead glaze compositions and alterations: example of Byzantine tiles.’ A. Bouquillon. C. Pouthas. Euro Ceramics V. Pt.2. Trans Tech Publications, Switzerland,1997, p.1487-1490 Quote: “A collection of architectural Byzantine tiles in glazed terra cotta is stored and exhibited in the Art Object department of the Louvre Museum as well as in the Musee de la Ceramique de Sèvres.”
- ↑ 'Industrial Ceramics.' F.Singer, S.S.Singer. Chapman & Hall. 1971. Quote: "The lighter pieces that are glazed may also be termed 'terracotta.'
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Terakota kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |