AFC Bournemouth
AFC Bournemouth ni klabu ya soka ya kulipwa yenye makao yake huko Kings Park, Boscombe, kitongoji cha Bournemouth, Dorset, Uingereza. Klabu hiyo inashiriki katika Ligi Kuu, ambayo ndio nafasi ya juu zaidi ya mpira wa miguu Uingereza.
Ilianzishwa mwaka wa 1899 kama Boscombe[1] , klabu ilipitisha jina lao la sasa mwaka wa 1971[2]. Kwa jina la utani "The Cherries", Bournemouth wamecheza mechi zao za nyumbani Dean Court tangu 1910. Rangi zao za nyumbani ni nyekundu na nyeusi,mashati yenye mistari, na kaptula nyeusi na soksi, iliyotokana na ile ya klabu ya Italia A.C. Milan.
Klabu ilishiriki katika ligi za kandanda za mikoa kabla ya kupanda kutoka ligi ya Hamphire hadi ligi ya kusini mwaka 1920. Sasa inajulikana kama Bournemouth & Boscombe Athletic, walichaguliwa kucheza ndani ya Ligi kuu ya Soka Uingereza mwaka wa 1923. Walibaki katika Ligi Daraja la Tatu Kusini kwa miaka 35, wakishinda Daraja ya Tatu Kusini mnamo 1946. Wakiwa wamepangwa upya katika ligi Daraja la Tatu mwaka wa 1958, walishuka daraja mwaka wa 1970, lakini walishinda nafasi ya kupandishwa tena daraja 1970–71. Timu hii ilirudishwa tena katika Ligi ya Ligi Daraja la Nne katika mwaka 1975, Bournemouth ilipandishwa daraja tena mwaka 1981-82 na baada ya kunyanyua kombe pa EFL katika fainali za 1984 na kuendea kushinda taji la Divisheni ya Tatu mnamo 1986-87. Walitumia misimu mitatu katika daraja la pili lakini waliingia katika mpira wa miguu wa Uingereza mwaka wa 1997 na wakaishia nyuma katika daraja la nne na kushuka daraja mwaka wa 2002, ingawa walipata kupanda daraja mara moja kwa kushinda mechi za mtoano mwaka 2003.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "AFC Bournemouth History". Bournemouth: AFC Bournemouth. 12 Mei 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Juni 2015. Iliwekwa mnamo 25 Juni 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "A F C Bournemouth". Football Club History Database. Richard Rundle. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Oktoba 2018. Iliwekwa mnamo 21 Juni 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu AFC Bournemouth kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |