Aleen Bailey
Aleen Bailey (alizaliwa 25 Novemba 1980, katika Saint Mary) ni mwanariadha wa kushindana wa kimataifa wa nchi ya Jamaica. Alishirika katika Olimpiki ya 2004 na akashinda medali ya dhahabu kama mwanachama wa timu ya mbio ya 4 x 100m. Bailey hufanya mazoezi katika Columbia, South Carolina chini ya kocha Curtis Frye na ni dada ya mwanamuziki maarufu wa rege Capleton.
Bailey alifuzu kutoka Chuo Kikuu cha South Carolina ambapo yeye alimaliza misimu iliyobaki baada ya kuhamia huko kutoka Chuo cha Jamii cha Barton.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Katika mashindano ya NCAA ya nje ya riadha,Bailey alishinda mbio ya 100m na 200m,akishinda aliyependelewa sana Muna Lee wa LSU. Alikuwa katika timu ya 4 x 100 katika mashindano ya mabingwa ya 2002.
Bailey alishindana kwa niaba ya nchi yake Jamaica katika Olimpiki ya 2004 alipomaliza katika nafasi ya 5 katika mbio ya 100m na nafasi ya 5 katika mbio ya 200m. Aliungana na bingwa wa mbio ya 200m,Veronica Campbell,Tayna Lawrence na Sherone Simpson na kushinda mbio ya 4 x 100m.
Katika Shindano la Dunia la Mabingwa katika riadha la 2005,alishinda medali ya fedha(akiwa pamoja na Daniele Browning,Sherone Simpson na Veronica Campbell)). Katika Michezo ya Pan Amerika ya 2007,alimaliza katika nafasi ya 5 katika mbio ya 200m na wakashinda medali ya dhahabu katika 4 x 100m.
Bailey aliwakilisha Jamaika katika Olimpiki ya 2008 mjini Beijing. Alishindana katika mbio ya 4 x 100m wakiwa pamoja na Shelly-Ann Fraser,Sheri-Ann Brooks na Veronica Campbell-Brown. Katika raundi ya kwanza, Jamaika ilikuwa ya kwanza mbele ya Urusi,Ujerumani na Uchina. Muda wao ulikuwa wa sekunde 42.24 uliokuwa bora kabisa katika mbio yote ya kuhitimu fainali. Kutokana na matokeo hayo,Jamaika ilhitimu kuingia fainali ambapo Bailey na Brooks waliwapa Sherone Simpson na Kerron Stewart nafasi zao katika timu. Jamaika haikumaliza mbio kutokana na makosa katika kubadilisha kijiti chao maalum kutoka mwanariadha mmoja hadi mwengine. [11]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Athlete biography: Aleen Bailey, beijing2008.cn, ret: 30 Agosti 2008
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- IAAF wasifu wa Aleen Bailey
- Biografia ya Bailey katika uscsports.com Archived 23 Machi 2006 at the Wayback Machine.
- Picha za Aleen Bailey