Beauveria
Beauveria | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Panzi waliouawa na Beauveria bassiana
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Beauveria ni jenasi ya kuvu entomopathojeni (kuvu zisababishazo magonjwa kwa wadudu) katika familia Cordycipitaceae. Kuvu hizi hazina jinsia na ni anamorfi za spishi za Cordyceps (teleomorfi zao). Spishi za Beauveria zinazaa spora nyeupe au njano ambazo ni ndogo sana na hazichanganyiki na maji. Zinazaliwa juu ya hife kwa umbo wa zigizaga.
Spishi za Beauveria huonekana sana zikimea juu ya mizoga ya wadudu. Zinatokea pia katika udongo kila mahali pa dunia, isipokuwa Antakitiki, na hata ndani ya mimea (endofiti). Spishi kadhaa, kama Beauveria bassiana na B. brongniartii, hutumika kama dawa za kibiolojia dhidi wadudu waharibifu.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]Tangu kuwadia kwa mihtasari ya jenetiki imewezekana kutambua spishi zaidi kuliko zamani. B. bassiana na B. brongnartii imeonekana kuwa michanganyiko ya spishi. Spishi mpya sita zimeeleza juzijuzi.
- Beauveria amorpha
- Beauveria asiatica
- Beauveria australis
- Beauveria bassiana
- Beauveria brongniartii
- Beauveria caledonica
- Beauveria kipukae
- Beauveria malawiensis
- Beauveria pseudobassiana
- Beauveria sungii
- Beauveria varroae
- Beauveria vermiconia
Spishi mbili zimewekwa katika jenasi nyingine: B. simplex inaitwa Acrodontium simplex sasa na B. nivea inaitwa Tolypocladium inflatum sasa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Hoog, G. S. d. 1972. The genera Beauveria, Isaria, Tritirachium, and Acrodontium gen. nov. Studies in Mycology 1:1-41.
- Shimazu, M., W. Mitsuhashi, and H. Hashimoto. 1988. Cordyceps brongniartii sp. nov., the teleomorph of Beauveria brongniartii. Transactions of the Mycological Society of Japan 29:323-330.
- Brady, B. L. K. 1979. Beauveria bassiana. CMI Descript. Pathog. Fungi Bact. 602:1-2.
- Li, Z., C. Li, B. Huang, and M. Fan. 2001. Discovery and demonstration of the teleomorph of Beauveria bassiana (Bals.) Vuill., an important entomogenous fungus. Chinese Science Bulletin 46:751-753.
- Rehner, S. A., and E. Buckley. 2005. A Beauveria phylogeny inferred from nuclear ITS and EF1-{alpha} sequences: evidence for cryptic diversification and links to Cordyceps teleomorphs. Mycologia 97:84-98.