Hori Kuu ya Australia
Hori Kuu ya Australia ni hori kubwa iliyopo upande wa kusini wa Bara la Australia.
Kuna namna tofauti za kuangalia sehemu hii ya bahari kati ya wataalamu wa Australia na wataalamu wa kimataifa.
Taasisi ya Hidrografia ya Autralia inafafanulia hivi:
Mipaka yake ni Rasi Pasley katika Australia ya Magharibi na Rasi Carnot katika Australia Kusini zilizo na umbali wa km 1,160.[1] Taasisi hii inatazama Hori Kuu ya Australia kuwa sehemu ya Bahari ya Kusini.
Shirika la Kimataifa la Hidrografia linaangalia eneo kubwa zaidi likitazama mstari baina ya Rasi ya Magharibi ya Howe (35°08′S 117°37′E) hadi Rasi ya Kusini Magharibi ya Kisiwa cha Tasmania kuwa mpaka wa kusini. Kwao hori ni sehemu ya Bahari Hindi.
Hakuna miji mikubwa kwenye pwani hiyo. Tabianchi ya pwani ni yabisi, sehemu kubwa ni tambarare inayoitwa "Nullarbor" inayomaanisha "pasipo miti",
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Great Australian Bight". Encyclopaedia Britannica. Iliwekwa mnamo 29 Septemba 2011.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)