Nenda kwa yaliyomo

Wakisi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wakisi ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Njombe, Wilaya ya Ludewa, ukanda wa Ziwa Nyasa

Lugha yao ni Kikisi.

Jamii hiyo hujihusisha na shughuli mbalimbali zikiwemo za uvuvi, ufinyanzi, kilimo cha muhogo.

Pia ni wachezaji wazuri wa ngoma ya Mganda, Kihoda na Ligambusi.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kwa mujibu wa mapokeo mbalimbali kabila la Wakisi wa nchini Tanzania ni asili moja na kabila la Wakisii wa nchini Kenya.

Wabantu wa kabila la Wakisi wanaonekana kuwa wa asili moja na Wabantu wa kabila la Wangoni kutokana na wote kuishi pamoja katika maeneo ya misitu ya Kongo kabla ya kutengana katika karne ya 8 BK ambapo Wangoni walipoelekea pande za kusini zaidi mwa bara la Afrika na kurejea tena katika makazi yao ya sasa kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Hivyo basi, makabila hayo mawili ya Wakisi na Wakisii asili yao ni moja ambapo katika lugha ya Kibantu waliitwa “Abhaghusuhi”. Watu hao waliitwa jina hilo kutokana na mbari ya mama yao aliyeitwa “Mughusuhi” kwa maana ya “Mkushi” kutoka nchini Ethiopia.

Huyo Mughusuhi alikuwa ni mke wa mfalme Sheba XXVIII ambaye alitawala upande wote wa kusini mwa bara la Afrika hadi kufikia miaka ya 829 BK aliporithiwa na mfalme Sheba XXIX ambaye pia alioa mwanamke Mkushi kutoka nchini Ethiopia na kuitwa “Mughusuhi” kwa lugha ya Kibantu.

Hivyo basi, kimsingi watu wa makabila hayO mbari yao ni Wabantu wa Kisheba ambao badala yake waliitwa kwa jina la mbari ya mama yao aliyeitwa “Mughusuhi” yaani “Mkushi”.

Mwaka wa 730 BK, Wakisii/Wakisi hao walikuwa miongoni mwa watu walioungana na vijana wa Kisuba waliosindikiza mgao wa urithi wa mali mtoto pekee wa kiume aliyeitwa “Umutusi” yaani aliyeachishwa ziwa iliyokuwa imekabidhiwa kwa mke wa mfalme Sheba XXIX aliyekuwa amefariki dunia kutokana na athari za vita ya Waarabu waliokuwa wamevamia na kutekA falme nyingi za kaskazini mwa bara la Afrika.

Wakisii/Wakisi hao walipata bahati ya kuteuliwa kuwa miongoni mwa wasindikizaji wa urithi huo wa mtoto “Umutusi” kwa kuwa mama ya hao Wakisii/Wakisi alikuwa wa kabila moja na mama yake huyo mtoto “Umutusi” ambaye mama yake aliitwa “Mughusuhi” yaani “Mkushi” aliyekuwa mke mdogo wa mfalme Sheba XXIX.

Katika karne ya 8 BK mwishoni, Wakisii/Wakisi haO ni miongoni mwa Wabantu wa mbari ya Wasuba ikiwa ni pamoja na watu wa koo za Abangoni, Ngoni, Isuru/Zulu, Sosa/Xhosa, Swazi, Ndebele na Chewa walioondoka katika misitu ya Kongo na kutawanyika katika mielekeo tofauti ambapo wengine wao walielekea pande za kusini zaidi mwa bara la Afrika, nyanda za juu kusini na wengine wakarejea makazi yao ya awali katika maeneo ya Nyancha/Nyansha (Viktoria Nyanza) ambako wanaishi hadi leo hii.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakisi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.