Nenda kwa yaliyomo

Wakwere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kinyago cha Kikwere

Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Wanakadiriwa kuwa zaidi ya laki moja.

Lugha yao ni Kikwere.

Wakwere hawana chifu kama makabila mengine ila wana msemi ambaye ndiye kiongozi mkubwa kwenye jamii yao. Wakwere wengi ni watawala yaani viongozi. Mfano ni Kikwete na Kidanga.

Kama Waluguru, Wakaguru, Wakutu na Wazaramo, kabila hilo linafuata mfumojike, yaani ukoo wa mama ndio unaoongoza familia na watoto wote wanahesabiwa kuwa wa ukoo huo.

Mila zao ni unyago kwa wanawake na jando kwa vijana wanaume waliobalehe. Hizo sherehe zinakuwa kubwa na za kupendeza.

Chakula cha asili cha Wakwere ni bambiko.

Baadhi ya sifa zao ni kuwa watu wastaarabu, wanakirimu sana wageni; Wakwere huona fahari pale ambapo nyumba yao imejaa wageni.

Historia inaonesha Wakwere walisafiri pamoja na Wazaramo na Wakutu kutoka nchi za mbali: makabila hayo matatu kwa kiasi kikubwa hawatofautiani mpaka lugha, siyo tu mila na desturi. Makabila hayo matatu hata baadhi ya majina wanachangia na yana asili kabisa kama Pazi, Shomvi n.k. Baadhi ya misamiati wanayotofautiana haitokani na msingi wa lugha bali inatokana na kuachana kimazingira baada ya kufika maeneo ya pwani. Wakutu wapo karibu zaidi na vijiji vya pwani vya Wazaramo hata kimaeneo.

Makabila hayo ni wacheshi na hupenda utani sana, pia ni watu wa majigambo na kujidai bila kiburi.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakwere kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.