Wasagara
Mandhari
Wasagara ni kabila la watu kutoka eneo la kati ya nchi ya Tanzania, hasa mkoa wa Morogoro, mpakani mwa mkoa wa Iringa kama Ruaha Mbuyuni, Mtandika na vijiji jirani, pembezoni mwa mto Ruaha na Mto Lukosi, wakilima vitunguu na kuviuza kwenye barabara kuu ya kwenda Zambia.
Mwaka 1987 idadi ya Wasagara ilikadiriwa kuwa 79,000 [1].
Lugha yao asili ni Kisagara, lakini wengi wao wanatumia zaidi lugha nyingine, k.mf. Kikaguru au Kihehe.
Wakiwa jamii ya Wakaguru, inasemekana jina linatokana na neno la Kikaguru wasigala (wamebakia) kwa kuwa ndio waliobaki Kilosa baada ya kutofika Milima ya Ukaguru.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wasagara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |