Einigkeit und Recht und Freiheit
Einigkeit und Recht und Freiheit ("Umoja na haki na uhuru") ni maneno ya kwanza ya wimbo wa taifa la Ujerumani. Wimbo huo ulitungwa kiasili na mshairi Hoffmann von Fallersleben mwaka 1841 kama "wimbo la Wajerumani" (Lied der Deutschen) likiwa na mabeti matatu. Lakini beti ya tatu pekee inayokubaliwa kama wimbo la taifa. Muziki yake iliandikwa na Joseph Haydn.
Beti asilia ya kwanza inajulikana kutokana na chanzo chake "Ujerumani juu ya yote" (Deutschland, Deutschland über alles) lakini baada ya maarifa ya utaifa mkali katika karne ya 20 uliopeleka nchi katika vita kuu mbili Wajerumani wengi hawapendi tena beti hii hivyo haitumiki tena.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Joseph Haydn alitunga muziki hii kwa heshima ya Kaisari Franz wa Austria na Dola Takatifu la Kiroma likawa wimbo la taifa la Austria hadi mwisho wa ufalme mwaka 1918.
Muziki latumiwa pia kwa nyimbo za kanisani katika nchi mbalimbali.
Mshairi August Heinrich Hoffman von Fallersleben alitunga shairi kwa ajili ya muziki hii mwaka 1841. Wakati huu Ujerumani iligawanyika katika madola mengi madogo. Kati ya wananchi hamu ilikuwa kubwa kuungana lakini wanasiasa katika kila sehemu hawakuona faida kuachana na hali halisi. Kwa wibo wake alitaja mipaka ya ameneo walipokaa watu waliosema Kijerumani katika madola mbalimbali, wengi ndani ya mipaka ya Shirikisho la Ujerumani lakini pia wengine nje yake. Alitaka kutamka tumaini alke wote wataunganishwa siku moja.
Baada ya vita mbili maeneo makubwa yaliyokaliwa na wasemaji wa Kijerumani wakati wa Hoffmann yako chini ya nchi nyingine na wakazi wa awali hawako tena; ama walizoea lugha nyingine au walifukuzwa hasa baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Kwa sababu hii majirani wa Ujerumani waliona maneno ya bei ya kwanza kwa mashaka, na Wajerumani wenyewe hawakutaka tena kuimba majina ya mito ambayao sasa ni sehemu ya mataifa mengine kwa hiyo hawatumii beti ya kwanza tena.
Katika karne ya 19 wimbo la Hoffmann lilipendwa na watu lakini halikuwa wimbo la kitaifa lililokuwa wimbo la kumsifu kaisari hadi 1918. 1922 lilitangazwa kuwa wimbo la taifa katika jamhuri ya Ujerumani; baada ya vita kuu ya pili rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani alitangaza beti ya tatu kama wimbo la taifa lakini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani walikuwa na nyimbo tofauti. Tangu 1990 beti la tatu ni wimbo la Ujerumani iliyounanika.
Maneno ya Kijerumani[hariri | hariri chanzo] |
Tafsiri kwa Kiswahili[hariri | hariri chanzo] |
Beti ya Kwanza[hariri | hariri chanzo] | |
|
|
Beti ya Pili[hariri | hariri chanzo] | |
|
|
Beti ya tatu - Wimbo rasmi la Taifa la Ujerumani[hariri | hariri chanzo] | |
|
|